Klabu ya Yanga imetambulisha Jezi ya tatu hadi sasa ikianzia na ile ya Mwanzo wa Msimu, halafu ikafuatiwa na ile ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere na hapo jana klabu hio imeongeza jezi nyingine na kufanya ifikie awamu tatu.
Utaratibu huo ndio unaifanya klabu hio iwe ya kwanza kuweka rekodi katika historia ya Michezo kwa klabu moja hapa nchini kutambulisha Jezi mara tatu mfululizo ndani ya msimu mmoja.
Aidha Rais wa klabu hio Hersi Said alibainisha kuwa Klabu ya Yanga imeingia mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Haier ambao una thamani ya Tsh. Bilion 1.5 kama mdhamini mkuu wa kombe la Shirikisho.“Young Africans SC imeingia mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5 kama mdhamini mkuu wa Kombe la shirikisho barani afrika” Rais Hersi Ally Said