Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane kwa ajili ya msimu ujao. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 huko Tottenham unaendelea hadi 2024 na anaweza kugharimu hadi euro 100m (£88.3m). (Todofichajes)
Poland wamewasiliana na kocha wa zamani wa Rangers na Aston Villa Steven Gerrard kuhusu kuwa meneja wao mpya. (Meczyki)
Arsenal wanafikiria kumnunua winga wa Real Madrid Eden Hazard, 32, ambaye alistaafu kucheza soka ya kimataifa akiwa na Ubelgiji mwezi Disemba. (Mediafoot)
Chelsea wameungana na Tottenham kutaka kumsajili beki wa Uhispania Pedro Porro mwezi huu lakini wamegonga suala sawa na Spurs katika harakati zozote za kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huku Sporting Lisbon wakitaka kipengele chake cha kuachiliwa cha €45m (£36.7m) kilipwe kikamili. (90Min)
Nottingham Forest pia wanavutiwa na mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Danjuma. (Sky Sports)
Atletico Madrid wanamtazama mshambuliaji wa Barcelona Mholanzi Memphis Depay, 28, kama mmoja wa wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Ureno Joao Felix, 23, ambaye anatazamiwa kujiunga na Chelsea kwa mkopo kwa muda wote uliosalia. (sportitalia.com)
Besiktas wamekubali kupokea takriban £2.7m kutoka Manchester United ili kumruhusu mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst, 30, kukatisha mkopo wake kutoka Burnley mapema na kuhamia klabu hiyo ya Old Trafford hadi mwisho wa msimu. Hata hivyo, upande waturuki hao wanataka kuwa na mbadala wake kabla ya kuruhusu hatua hiyo. (Guardian)
Creddit; BBC Swahili