ADVERTISEMENT
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemhukumu Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake wanne kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kuwakuta na hatia katika makosa mawili kati ya matatu kwenye kesi ya jinai namba 10/2022 huku wafuasi wengine wanne wakiachiwa huru.
–
Mahakama imesema Mfalme Zumaridi atatumikia mwezi mmoja katika gereza kuu la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa huku wenzake wanne wakitumikia kufungo cha mwaka mmoja nje ya gereza.
–
Credit : #EastAfricaTV
ADVERTISEMENT