Shirika la Ndege Nchini, Precision Air limeujuza umma hii leo Februari 3,2023 kuwa moja ya ndege zake imepatwa na hitilafu za kiufundi hadi kupelekea kuahilishwa kwa ratiba ya safari iliyotakiwa fanyika kupitia ndege hio.
ADVERTISEMENT
Aidha ndege yake nyingine yenye Usajili 5H-PWD imekubwa na madhira baada ya kukonga ndege (mnyama) pindi inaruka kwa safari yake kutokea Dar kuelekea Dodoma hivyo kulazimika kutua kwa dharura ili kupuka taharuki zaidi.
Shirika hilo limeomba radhi kwa wateja wake juu ya usumbufu uliojitokeza na kuahidi kufanyika kazi masuala hayo ili huduma zake ziweze rejea kama kawaida.