Mwimbaji wa Nigeria Tems alishinda tuzo ya Grammy siku ya Jumapili – na kuwa msanii wa kwanza wa kike kutoka nchini humo kushinda tuzo hiyo ya kifahari.
Mwenzake Burna Boy alishindwa katika kategoria mbili alizoteuliwa. Tems, ambaye jina lake halisi ni Temilade Openiyi, alishinda tuzo katika kitengo cha Best Melodic Rap Performance kutokana na mchango wake katika wimbo wa Wait for U – alioshirikiana na wanamuziki Future na Drake.
Congrats Best Melodic Rap Performance winner –
"WAIT FOR U" @1future ft. @Drake & @temsbaby #GRAMMYs
🎶 WATCH NOW https://t.co/PMy5r3LaPU pic.twitter.com/GUSnjDI5aB— Recording Academy / GRAMMYs (@RecordingAcad) February 5, 2023