ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Mwanaume mmoja amefariki dunia katika Kisiwa cha Puerto Rico baada ya kuanguka kutoka kwenye mwamba wenye urefu wa futi 70 wakati akirekodi video ya Tik Tok.
–
Kwa mujibu wa familia yake, Edgar Garay (27) kutokea Indiana alikuwa kwenye safari ya mapumziko, na mwili wake ulipatikana siku moja baada ya ajali hiyo iliyotokea Januari 29.
–
Kaka wa marehemu Carlos Garay amesema kuwa “kaka yangu alikuwa na akaunti Tik Tok ,ambapo alipenda kuposti video, kwa bahati mbaya hicho ndicho alichokuwa akijaribu kufanya, lakini alikuwa amesogea mno ukingoni mwa mwamba.”
–
Familia yake iko kwenye zoezi la kukusanya michango kupitia akaunti iliyothibitishwa kwenye mtandao wa GoFundMe ili kuweza kuusafirisha mwili wa mpendwa wao kwenda nyumbani kwao Indiana kwa ajili ya mazishi.