Mtu mmoja amefariki dunia na wengine saba wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara, kwa madai ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kuregee wilayani Serengeti, ambapo watu hao wa familia moja wanadaiwa kula chakula hicho usiku wa Februari 3, 2023, chakula ambacho ni ugali, nyama ya sungura na maziwa, na ilipofika alfajiri walianza kuhara na kutapika.
–
Kwa mujibu wa baba wa familia hiyo Abbas Musoma, waliokula chakula hicho walikuwa watu 9 lakini mmoja hakupata madhara makubwa, 8 wakizidiwa na mmoja kati yao amefariki dunia.
–
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya ndani katika hospitali ya mkoa wa Mara Dkt. Edibili Mtatiro amesema alipokea watu saba na mwili mmoja na kwamba hali za wagonjwa hao saba zinaendelea vizuri.