Msemaji wa Klabu ya Hatayspor ya Uturuki, Mustafa Ozat, amethibitisha kuwa winga wa klabu hiyo, Christian Atsu amepatikana akiwa hai na anaendelea na matibabu kutokana na kujeruhiwa mguu na amepata pia tatizo la kupumua vizuri.
–
Winga Huyo wa zamani wa Chelsea na Newcastle ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya Uturuki ya Hatayspor, alikuwa miongoni mwa wale ambao walikuwa hawakujulikana walipo baada ya tetemeko lililotokea nchini uturuki na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 4800.
–
Ozat amekiambia chombo cha Habari kutoka Uturuki, Radyo Gol kuwa Atsu aliondolewa kwenye moja ya vifusi vya majengo yaliyoanguka kutokana na tetemeko lakini akaweka wazi kuwa Mkurugenzi wao wa michezo, Taner Savut, bado yuko chini ya kifusi hajapatikana.