Mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na dansa Beyoncé Giselle Knowles-Carter kutoka nchini Marekani amekuwa msanii wa kwanza kutunzwa zaidi katika historia ya tuzo za Grammy.
–
Mpaka sasa Beyoncé ameshinda mara 32 katika tuzo hizo. Tuzo iliyomweka Beyoncé juu zaidi ilikuwa albamu bora ya densi/elektroniki ambayo ameshinda kutoka kwenye albamu yake ya ‘Renaissance’.
–
Tuzo za Grammy kwa mwaka 2023 zimefanyika Jumapili Februari 5, 2023 nchini Marekani ambapo Beyoncé alijizolea ushindi wa tuzo nyingine mbili, Best R&B Song (Cuff It), Best Traditional R&B Performance (Plastic Off The Sofa)
ADVERTISEMENT