Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemtangaza Mchezaji Bruno Gomez anayekipiga mnamo kikosi cha Singida Big Stars kuwa ndio Mchezaji Bora wa Mwezi Januari Ligi Kuu ya NBC 2022/2023.
Nyota huyo wa Brazil amekuwa na nafasi ya pekee kwa kushinda tuzo akicheza kwa mara ya kwanza na msimu wa kwanza kwake katika Ligi kuu na ikiwa ni bado mapema kabisa msimu wa mwaka huu kutamatika.
Aidha imeongeza kwa kumtaja kocha mkuu anayekinoa kikosi hicho alipotokea mchezaji bora wa Mwezi Hans Van Pluijm kuwa ndio Kocha bora wa Mwezi huo Januari pia.
Kocha Pluijm amewashinda Makocha wawili wa Timu ya Simba Robetinho na Yanga Nabi kutokana na kufanya vema zaidi katika michezo ya mwishoni kabisa wa mwezi jJanuari na kuonekana bora katika msimamo wa ligi.