Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema ATCL ina madeni ya zaidi ya Sh4.86 bilioni yanayotokana na kutowasilishwa michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hali inayosababisha kutolipwa kwa wastaafu wa ATCL
–
Mwakibete ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalumu Angelina Malembeka (CCM) amehoji ni lini Wastaafu wa ATCL watalipwa mafao yao ambayo wamekuwa wakiidai Serikali kwa muda mrefu
–
“Kwa kuzingatia uhakiki uliofanyika, ATCL ina madeni ya zaidi ya Sh4.86 bilioni yanayotokana na kutowasilishwa michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,” amesema Mwakibete