ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, April 2, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Dkt. Jafo: “Huenda zaidi ya Sh. Trilioni 1 Zikapatikana kwa Mwaka Kutokana na Biashara ya Kaboni”

Dodoma

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Feb 3, 2023
in HABARI
0
Dkt. Jafo: “Huenda zaidi ya Sh. Trilioni 1 Zikapatikana kwa Mwaka Kutokana na Biashara ya Kaboni”
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

DKT. DUGANGE- BILIONI 69.95 ZIMETENGWA KUNUNUA VIFAA TIBA NCHINI

DKT. DUGANGE- BILIONI 69.95 ZIMETENGWA KUNUNUA VIFAA TIBA NCHINI

Feb 9, 2023

Bilioni 213 za Miradi ya DMDP Zaistawisha Temeke

Feb 2, 2023

DKT. DUGANGE-95% YA ZABUNI ZA TARURA KAZI INAENDELEA

Jan 24, 2023
Load More
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema huenda zaidi ya sh. trilioni moja zikapatikana kwa mwaka kutokana na biashara ya kaboni.
Mhe. Jafo ametoa wito kwa wabunge kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kushiriki katika biashara hiyo kwa kupanda miti kwa wingi hatua itakayosaidia katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ametoa kauli hiyo Februari wakati akichangia taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma Februari 01, 2023.
Amewataka Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) kuongeza nguvu katika kuhakikisha misitu yote inatunzwa, badala ya kukatwa kwa ajili ya kuni, mkaa au matumizi mengine badala yake sasa misitu hiyo itatumika katika biashara ya kaboni
Dkt. Jafo amesema miongoni mwa maeneo ambayo yameanza kunufaika na biashara ya kaboni ni pamoja na Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi ambayo kwa wastani kwa mwaka inapata takriban sh. bilioni 2 hadi 3 hivyo ametoa hamasa kwa wilaya zingine kuhakikisha wanatunza misitu kwa ajili ya biashara hiyo.
“Niwaombe ndugu zangu wabunge tupitie kanuni na mwongozo wa kusimamia biashara ya kaboni hii itasaidia sana hasa katika kuhakikisha maeneo yetu na kuona jinsi gani tunayaelekeza hasa katika suala zima la kuvuna hewa ukaa,” amesisitiza.
Aidha, Waziri Jafo amesema biashara ya kaboni itagusa TFS ambao wana dhamana ya kuhifadhi misitu na kilimo (agro-forest) kwa wakulima wanaojihusisha na kilimo cha mikorosho, miparachichi na kahawa.
Katika hatua nyingine Dkt. Jafo amewapongeza wananchi kwa kuiunga mkono Serikali kwa kuchukulia ajenda ya kuhifadhi mazingira katika umuhimu wake kwa kuhakikisha wanapanda miti na kuitunza.
Awali akichangia katika taarifa hiyo Mbunge wa Kuteuliwa Mhe. Liberata Mulamula ametoa wito kwa Serikali kuchangamkia fursa ya kupata fedha za mabadliko ya tabianchi zinazotolewa na nchi zilizoendelea kwa nchi zinazoendelea
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: OFISI YA RAIS TAMISEMI
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

EX MSUMBUFU KUFUNGWA JELA MIAKA MITANO
HABARI

EX MSUMBUFU KUFUNGWA JELA MIAKA MITANO

by Shabani Rapwi
Apr 2, 2023
CAMERA ILIYOPOTEA MIAKA 13 YAPATIKANA KWENYE MATOPE PICHA BADO ZIPO VIZURI
HABARI

CAMERA ILIYOPOTEA MIAKA 13 YAPATIKANA KWENYE MATOPE PICHA BADO ZIPO VIZURI

by Shabani Rapwi
Apr 2, 2023
AFUKUA MAITI YA MAMA YAKE NA KUKAA NAYO NDANI
HABARI

AFUKUA MAITI YA MAMA YAKE NA KUKAA NAYO NDANI

by Shabani Rapwi
Apr 2, 2023
MUUGUZI AFARIKI AKIJIFANYIA HUDUMA MWENYEWE
HABARI

MUUGUZI AFARIKI AKIJIFANYIA HUDUMA MWENYEWE

by Shabani Rapwi
Apr 2, 2023
CHINA NA BRAZIL ZAIKATAA DOLA YA MAREKANI
HABARI

CHINA NA BRAZIL ZAIKATAA DOLA YA MAREKANI

by Shabani Rapwi
Apr 2, 2023
YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI
HABARI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
February 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728  
« Jan   Mar »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In