Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi hatokuwa Airpot kwani tayari yupo nchini Tunisia.
–
“Tunaondoka Dar Es Salaam leo saa 9:25 alasiri kuelekea Dubai, ambapo tutapumzika hapo na kesho tutaondoka kuelekea Tunisia, tunasafiri na wachezaji 25 na benchi la ufundi 6 pamoja na Aboutwalib Mshery akienda kwa ajili ya matibabu na Mwalimu Nabi akiwa ameshatangulia Tunisia kwa ajili ya maandalizi” amesema Ally Kamwe.
–
Wachezaji wa Yanga watawasili kesho nchini Tunisia kwa ajili ya mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir itakayochezwa Jumapili.