Idadi ya waliofariki katika ajali ya barabarani wilayani Korogwe imefikia 20 baada ya majeruhi watatu waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufariki dunia leo.
–
Taarifa za vifo vya majeruhi hao zimethibitishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kalist Lazaro.
–
Katika ajali hiyo iliyotokea eneo la Magira Gereza, Tarafa ya Mombo, wilayani Korogwe, watu 17 walifariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa.
–
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni Mitsubish Fuso iliyogonga gari aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26, ikitokea Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.