Nyota wa Los Angeles Lakers, LeBron James amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa NBA baada ya leo Alfajiri kufunga pointi 38 katika mechi iliyowakutanisha Lakers dhidi ya Thunder.
–
Baada ya kufunga pointi hizo LeBron James amefikisha pointi 38390 na kumpita Kareem Abdul Jabbar aliyekuwa anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa NBA kwa pointi 38387 rekodi aliyoiweka mwaka 1984.
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Kareem Abdul Jabbar naye ni nguli katika timu ya Los Angeles Lakers ambapo aliichezea kuanzia mwaka 1975 – 1989 na leo alikuwepo uwanjani kushuhudia rekodi mpya ikiwekwa.