ADVERTISEMENT
Mwanamke mmoja raia wa Kenya anayeishi nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha miezi 44 jela na faini ya dola za Kimarekani milioni moja kwa ushiriki wake kwenye ulaghai wa mahusiano ya kimapenzi pamoja na utapeli kipindi cha corona.
–
Florence Mwende Musau (38) alihukumiwa wakiwemo watu wengine watano kuhusiana na kulaghai watu kwa njia ya mtandao ambapo waathirika wa utapeli huo walipoteza takribani dola za Kimarekani milioni 4.
–
Kwa mujibu wa Mamlaka za nchini Marekani wahusika walitumia pasipoti feki na nyaraka nyingine feki kufungua akaunti za benki ndani na nje ya jiji la Boston. Akaunti hizo zilitumika kukusanyia pesa katika ulaghai wa mahusiano ya kimapenzi.
–
Vilevile Musau alikuwa akipokea msaada wa pesa kutoka Serikalini kwa kutumia majina ya watu wengine. Msaada huo ulilenga kuwasaidia watu waliopoteza kazi kipindi cha corona.
–
Taarifa zinaeleza kuwa, Musau pekee alikuwa akimiiki akaunti 10 feki za benki ambazo alikusanyia takribani dola za Kimarekani milioni moja.
ADVERTISEMENT