Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, Babu Sikare almaarufu Albino Fulani amefariki dunia.
–
ADVERTISEMENT
Taarifa za kifo chake, zimetolewa na mmoja kati ya marafiki zake wa karibu na msanii mwenzake, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kupitia ukurasa wake wa Twitter.
ADVERTISEMENT
–
Taarifa za awali, zinaeleza kuwa Albino Fulani amefia Columbus, Ohio nchini Marekani alikokuwa akiishi.