Jeshi la Polisi mjini Durban nchini Afrika Kusini limethibitisha kuwa mwanamuziki Kiernan Forbes maarufu AKA alipigwa risasi na kufa katika barabara ya Florida usiku wa kuamkia leo.
–
Mtu mwingine anayeaminika kuwa mlinzi wa msanii huyo pia alijeruhiwa, huku mtu mwingine ambaye hajajulikana, ambaye inafahamika kuwa rafiki wa karibu na AKA, ameuawa kwa kupigwa risasi pia.
–
Taarifa ya Polisi inasema AKA alikuwa amesimama nje ya Mkahawa wa Wish alipopigwa risasi kwenye gari. Magari mawili yasiyojulikana yanaaminika kufyatua risasi.
–
Kwa mujibu wa post za mitandao ya kijamii, AKA alitakiwa kutumbuiza kwenye club ya Durban, YUGO, ambapo alitarajiwa kutumbuiza ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
–
Enzi za uhai wake AKA mwenye umri wa miaka 35 aliwahi kufanya wimbo na msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz unaoitwa Make Me Sing, Video ya wimbo huo iliachiwa rasmi Februari 12, 2016 ambapo mpaka sasa inawatazamaji Milioni 13. (13M views) kwenye mtandao wa YouTube.