Mwigizaji wa filamu, mwanamitindo na mjasiriamali nchini, Jacqueline Wolper azungumzia tetesi za mitandaoni kuwa mume wake ana mtoto mwingine wa tatu nje ya ndoa tofauti na wawili waliozaa pamoja. Wolper alipoulizwa amejibu.
–
“Kuhusu mtoto wa tatu siwezi kuongelea chochote kwasababu kitanda hakizai haramu, na Yule ni mwanaume kama ameweza kupiga wawili kwangu why not watatu.
–
Lakini sio vitu vya kuongelea sana kama mtoto yupo atajulikana, ukweli haujifichi unajua mie ni mke wa ndoa halafu vitu kama hivyo siwezi kuongelea sana. Mie ni mwanamke najua uchungu wa mtoto siwezi kuongelea kwa ubaya wala kwa uzuri.
–
Vitu ambavyo sijaambiwa na mume wangu huwa sipendi kuvifatilia tumefundishwa hivyo katika mafundisho ya ndoa. siku akija kuniambia nitakuja kuwaambia na nitakwambia nimeamua nini”