ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, March 22, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda

I am Krantz by I am Krantz
Feb 3, 2023
in BIASHARA, MICHEZO
0
NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

NA MWANDISHI WETU

RelatedPosts

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

Mar 21, 2023

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

Mar 21, 2023

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

Mar 21, 2023
Load More

BENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo kwa Viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Wafanyabiashara Wadogo (Machinga) na Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, wanaoondoka nchini Jumatatu Februari 6, kwenda Kigali, Rwanda.

NMB imekabidhi tiketi 12 za kwenda na kurudi Rwanda kwa wajasiriamali hao 10 na viongozi wawili, watakaoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro na Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Dk. Elizabeth Mshote.

ADVERTISEMENT

Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, ambako Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa, alimkabidhi tiketi hizo Mkuu wa Mkoa, Mhe. Amos Makalla, ambaye ni mbunifu wa wazo la kupeleka viongozi hao Kigali, kujifunza namna sahihi za kuendesha biashara zao na Sekta ya Usafirishaji wa bodaboda.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kuwaaga, RC Makala aliipongeza NMB kwa kukubali kufadhili safari ya viongozi hao wa makundi hayo muhimu katika mpango mkakati wake wa kuipandisha Dar es Salaam kutoka nafasi ya sita kwa usafi barani Afrika, kuwa namba moja – inayoshikiliwa na Kigali hivi sasa.

“Nilipotembelea Rwanda, nikashawishika kutuma wawakilishi wa kwenda kujifunza na nikawasilisha wazo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alilikubali na kulibariki. Bahati mbaya sikuwa na fungu la kufanikisha ziara yao. Nashukuru NMB ikalipokea hili na kufanya uwezeshaji huu ambao unaunga mkono jitihada za Serikali.

“Ni wazo lililokuwa linaunga mkono jitihada za Rais Samia ambaye alikutana na Machinga Ikulu na kupanga nao mikakati ya kuboresha mazingira ya utendaji kazi wao na kuleta tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Leo tunakabidhiwa tiketi na Jumatatu nitawasindikiza Uwanja wa Ndege mimi mwenyewe,” alisisitiza Makala.

Aliwataka viongozi hao kuitumia vema ziara hiyo kwa kuhakikisha wanajifunza mbinu sahihi za uendeshaji shughuli katika mazingira yasiyokwaza Mamlaka na Jamii, sanjari na kuwa mabalozi wema watakaovutia Wanyarwanda nao kuja kujifunza katika maeneo mengine na kushirikiana nao kibiashara.

Kwa upande wake, Baragomwa alisema siri ya NMB kuitikia haraka maombi ya kuwezesha ziara hiyo ni udau mkubwa ilionao kwa maendeleo ya jamii, hivyo walilipokea ombi hilo kama jukumu lao la kuinyanyua kada hiyo ya Machinga na Bodaboda kibiashara na kiuchumi.

Mbele ya Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, Baragomwa akasisitiza kuwa benki yake inajivunia ushirikiano baina yao, Serikali na jamii, alioutaja kuwa umechangia faida kubwa ya Sh. Bilioni 429 kwa mwaka 2022, pato lililotanua fungu la Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kufikia Sh. Bilioni 6.2.

Alibainisha kuwa, kupitia ziara hiyo, viongozi hao watajifunza mengi nchini Rwanda, ambako nao wametuma wawakilishi wawili, huku akiwahakikishia huduma bora na rafiki pindi watakaporudi zikiwemo za NMB MastaBoda na mikopo yenye riba nafuu kwa Machinga na wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa.

Aidha, DC Mpogoro alimshukuru RC Makala kwa wazo lake hilo linaloenda kumaliza changamoto za kiutawala dhidi ya makundi hayo, huku Mwenyeviti wa Machinga Dar, Namoto Yusuph na wa Bodaboda Dar, Saidi Chenja, wakiiahidi NMB na Serikali kutumia ziara hiyo kwa ustawi wa shughuli zao na miundombinu ya Jiji na usafi wa mazingira.

…. The End…..

ADVERTISEMENT

 

 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’
MICHEZO

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
HAALAND KUIKOSA HISPANIA
MICHEZO

HAALAND KUIKOSA HISPANIA

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
MUSONDA AHUSIKA ZAIDI YANGA KUTINGA ROBO FAINALI CAFCC
MICHEZO

MUSONDA AHUSIKA ZAIDI YANGA KUTINGA ROBO FAINALI CAFCC

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
YANGA YAFANYA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU DAR
MICHEZO

YANGA YAFANYA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU DAR

by ALFRED MTEWELE
Mar 17, 2023
MSEMAJI SINGIDA BS AKANUSHA BRUNO KUTUA YANGA
MICHEZO

MSEMAJI SINGIDA BS AKANUSHA BRUNO KUTUA YANGA

by ALFRED MTEWELE
Mar 17, 2023
RASHFORD AJIWEKEA REKODI NZURI BARANI ULAYA
MICHEZO

RASHFORD AJIWEKEA REKODI NZURI BARANI ULAYA

by ALFRED MTEWELE
Mar 17, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
February 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728  
« Jan   Mar »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In