ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, March 22, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

PROF. MAKUBI ATAKA WANANCHI WAJUE UMUHIMU WA CHANJO

Dodoma

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Feb 2, 2023
in HABARI
0
PROF. MAKUBI ATAKA WANANCHI WAJUE UMUHIMU WA CHANJO
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

SERIKALI YATANGAZA KUZUKA KWA UGONJWA USIOJULIKANA KAGERA

SERIKALI YATANGAZA KUZUKA KWA UGONJWA USIOJULIKANA KAGERA

Mar 17, 2023

YASTAAJABISHA: VIJANA WANAHITAJI UZA FIGO ZAO

Mar 13, 2023

MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE KIKWAZO TENA

Feb 9, 2023
Load More
May be an image of 1 person, standing and sittingKATIBU MKUU Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Waratibu wa Chanjo nchini kuimarisha utoaji elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya magonjwa.
Prof. Makubi amesema hayo jana Februari 1, 2023 wakati akifunga kikao kazi cha tathmini ya kampeni ya Chanjo ya polio awamu ya nne kilicho hudhuriwa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Waratibu wa chanjo pamoja na Wadau mbalimbali katika Sekta ya afya.
“Niendelee kutoa wito kwenu nyote kutoa elimu kwa wananchi wote na kuwajuza juu ya umuhimu wa chanjo ili kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.” Amesema Prof. Makubi.
Sambamba na hilo Prof. Makubi amewaagiza wataalam hao kwenda kusimamia uchanjaji wa chanjo ya Polio na kuhakikisha huduma za chanjo kwa njia ya mkoba zinafanyika na kuwafikia watoto wote ambao hawajapata au kukamilisha ratiba ya chanjo.
Aidha, Prof. Makubi amewataka kuhakikisha wakati wanapopambana kuongeza uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19 huduma zingine za Afya ikiwemo chanjo za watoto ziendelee kutolewa vyema ili kutoruhusu milipuko ya magonjwa mengine hasa yaliyokwisha kupunguzwa au kutokomezwa.
Pia, amesema, Ili tuweze kuzuia ongezeko la wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni vyema kuweka mikakati ya kuongeza kiwango cha uchanjaji wa chanjo hii kupitia vikao vya usimamizi wa huduma za Afya vya Mikoa na Halmashauri ili kufikia mwisho wa mwaka 2023 kila mkoa uweze kuvuka lengo la asilimia 95 ya uchanjaji wa chanjo hii na chanjo zingine zote.
Pamoja na hayo, Prof. Makubi amewataka Wataalamu wote kujikita katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote itayomsaidia kila mwananchi kupata matibabu bila malipo kuanzia ngazi ya Zahanati mpaka hospitali ya Taifa.
Lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuhakiksha kila mwananchi anapata huduma bora na salama pasipo usumbufu, ujio wa bima ya Afya kwa wote utaweza kusaidia kuwa na huduma endelevu zikiwemo za chanjo zisizotegemea wadau katika uendeshaji wake pindi watakapo sitisha ufadhili wao. Amesisitiza Prof. Makubi.
Akitoa salamu kwa niaba ya Waganga wakuu na Waratibu wa Chanjo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Best Magoma amesema, jitihada kubwa za utoaji chanjo kwa wananchi tayari zimefanywa na zimesaidia kuwakinga wananchi kwa kiasi kikubwa.
Sambamba na hilo amemshukuru Katibu Mkuu kwa kuendelea kusimamia upatikanaji wa huduma bora ikiwemo upatikanaji wa Chanjo huku akimuahidi Wataendelea kushirikiana na Wataalamu wengine katika ngazi zote ili kuwakinga wananchi dhidi ya magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Polio.
Mwisho.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: Wizara ya Afya
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI
HABARI

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA
HABARI

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI
HABARI

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
BIKIRA JANE APATA MTOTO
HABARI

BIKIRA JANE APATA MTOTO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA
HABARI

ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO
HABARI

SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
February 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728  
« Jan   Mar »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In