Mkufunzi wa zamani wa timu ya Taifa Misri na Africa Kusini (Bafana Bafana), Carlos Queiroz ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Qatar
–
ADVERTISEMENT
Queiroz ambaye amewahi kuhudumu kama kocha msaidizi wa Sir Alex Ferguson kunako Manchester United alikuwa kocha wa Iran kwenye michuano ya kombe la Dunia 2022.
–
ADVERTISEMENT
Queiroz (69) raia wa Ureno pia amewahi kuwa kocha klabu ya Real Madrid, timu za Taifa Ureno, Colombia na Saudi Arabia.