Rais wa zamani wa Pakistan, Jenerali Pervez Musharraf amefariki dunia leo Februari 5, 2023 akiwa na umri wa miaka 79.
–
Musharraf aliyefanya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1999 amefariki huko Dubai alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu, taarifa ya jeshi imesema.
–
Alishika wadhifa wa urais rasmi kati ya mwaka 2001 hadi 2008 aliposhindwa kwenye uchaguzi mkuu na aliondoka nchini Pakistani miezi sita baadaye.
–
Alirudi tena nchini Pakistan mwaka 2013 na kujaribu kugombea tena urais, alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhaini na alihukumiwa kifo bila yeye kuwepo, hata hivyo hukumu hiyo ilibadilishwa mwezi mmoja baadaye.
–
Aliondoka Pakistan mwaka 2016 kutafuta matibabu na amekuwa akiishi huko tangu mwaka huo hadi mauti ilipomkuta.