ADVERTISEMENT
Uhamisho wa winga wa Chelsea Hakim Ziyech kujiunga na PSG kwa mkopo umeshindwa kukamilika baada vilabu hivyo kushindwa kusaini mikataba kwa wakati kutokana na kuchelewa kwa nyaraka kutoka Chelsea na kusababisha dirisha la usajili kufungwa huku saini zikiwa hazijakamilika.
–
Inaelewa nyaraka hizo zilichelewa kutokana na Chelsea kutuma nyaraka zisizo sahihi mara kadhaa na kupelekea kuchelewa na hatimaye kukwamisha uhamisho wa nyota huyo raia wa Morocco ambaye atalazimika kusalia darajani Stamford Bridge.
–
Vilabu hivyo vilikamiliisha mazungumzo kwa ajili ya mkataba wa mkopo usio na changuo la kumnunua jumla. Ziyech alitua Paris tayari kwa vipimo vya afya huku vilabu vikiendelea na mazungumzo, lakini mwishowe mambo yalikwenda mrama.
ADVERTISEMENT