Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba SC, Salim Muhene (Try Again) baada ya kushiriki moja ya vipindi vinavyoendelea kwenye kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika mjini Tangier, Morocco.
Try Again ni mmoja wa wajumbe watatu kutoka Afrika ambao wanashiriki kozi hiyo ambapo kwa upande wa Afrika Mashariki alichaguliwa yeye peke yake. Huu ni mwendelezo wa FIFA kutoa kozi hiyo kwani ilianzia nchini Qatar wakati Kombe la Dunia likiendelea ambako pia Try Again alishiriki.
Related