Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Muhene (kulia) baada ya kushiriki moja ya vipindi vinavyoendelea kwenye kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu (Diploma in Club Management) inayotolewa na FIFA inayofanyika mjini Tangier, Morocco.
–
Muhene, maarufu Try Again, ni mmoja wa wajumbe watatu kutoka Afrika ambao wanashiriki kozi hiyo ambapo kwa upande wa Afrika Mashariki ndiye aliyechaguliwa.
–
Huu ni mwendelezo wa FIFA kutoa kozi hiyo ambayo ilitolewa pia nchini Qatar wakati Kombe la Dunia.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT