Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewaonya Vijana kuacha kubahatisha maisha kwa kuendekeza kucheza kamari (Ku-Bet) na badala yake ameaataka wajifunze ujuzi mbalimbali ili wajiajiri na kukuza uchumi wao.
–
Kauli hiyo ameitoa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki “Maisha sio kubahatisha, mnakuwa Watumwa, tafuteni Vyuo vya Ufundi kama VETA mpate maarifa mjiajiri, najua wengi hawatafurahishwa na hili lakini huo ndio ukweli”
–
“Vijana siku nzima bize kwenye mkeka, Bet, unajiuliza hivi Kijana wewe , Kijana rijali kabisa mzima una mwili wenye nguvu, unakaa unasubiria eti niandike kwenye karatasi Timu fulani na Timu fulani itashinda hii, ili uishi”
–
“Sasa najua kuna Watu nawaharibia biashara lakini lazima tuambiane ukweli, tuachane na mambo ya kuishi kwa bahati nasibu tuchonge laini fanya biashara inayokupa matokeo mwishoni, achana na hii unatafuta Elfu 20 kila siku kwenda kumpatia Mtu mwingine anapata huko wewe unabakia unapiga miayo”