Walimu sita kutoka Kaunti ya Kisii nchini Kenya wametiwa mbaroni kwa video ya kutatanisha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo watoto wa shule wanaswa wakifanyiwa kitendo kichafu.
–
Akithibitisha kukamatwa kwa walimu hao watano wa kike na mmoja wa kiume, OCPD wa Nyamache Kipkulei Kipkemboi alisema kisa hicho kilitokea katika Shule ya Msingi ya Itumbe DOK huko Nyamache.
–
Walimu hao ni, Everline Moraa, Gladys Kenyanya, Angelicia Joseph, Moraa Nyairo, Cathrine Mokaya na William Isoka, walikamatwa baada ya maafisa wa Wizara ya Elimu katika kaunti hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kaunti Ndogo ya Nyamache Linet Onduso kuzuru shule hiyo baada ya kupokea klipu hiyo.

Katika video hiyo ambayo imezua taharuki kwa umma, watoto hao wa kiume waliovalia sare za shule wanalazimishwa na walimu wao kufanya kitendo kichafu huku wakiwa wamelala juu ya kila mmoja huku walimu wakicheka kwa sauti ya chini kwa nyuma.
–
Kulingana na OCPD, walimu hao sita wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Nyamache wakisubiri kufikishwa Mahakamani.
–
Chanzo : Citizen TV Kenya
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT