Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amewasimamisha kazi watumishi wa umma wawili wilayani Korogwe ili kupisha uchunguzi wa sababu za wao kuchelewa kufika eneo la tukio baada ya ajali kutokea wilayani Korogwe mkoani Tanga.
–
Mgumba ametoa kauli hiyo wilayani Korogwe baada ya kuzungumza kwa undani na watumishi pamoja na ndugu wa marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
–
Waliosimamishwa kazi ni mganga mkuu wa halmashauri ya mji Korogwe, Salma Swedi na mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Magunga, Korogwe Dkt. Heri Kiwale.
–
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 4 na nusu usiku hapo jana na watumishi wa hospitali hiyo walifika eneo la tukio saa kumi kasoro alfajiri hii leo.