WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa jamii kutojihusisha na kurekodi mattukio na kurusha mitandaoni bali wapeleke katika mamlaka husika ili hatua za kisheria ziweze chukuliwa dhidi ya wahusika.
Majaliwa ameeleza hayo leo Bungeni jijini Dodoma akitolea ufafanuzi juu ya Makosa ya Walimu kutoa Adhabu kali kwa wanafunzi ambazo zinaweza wapelekea kupata majeraha ya kudumu au athari kubwa zaidi za kiafya.
Hilo limezungumziwa kwa kuhusianiswa na tukio lililojitokeza hapo siku chache kupitia klipu ya Video iliyovuma sana ikimuonesha Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya huko mkoan Kagera akimuadhibu Mwanafunzi vikali na huku akiwa amemkanyaga katika sehemu ya mguuni.
Kitendo hicho kilipelekea hali ya taaruki kwa jamii nzima nchini kuona mtoto mdogo akipatiwa adhabu kuzidi hata umri wake, ndipo serikali ikaingilia kati kwa kutoa tamko la kumsitisha kazi Mwalimu huyo na hatua nyingine za kisheria ziweze chukuliwa dhidi yake.
Zifuatazo zilikuwa ni sehemu ya nukuu za Waziri Mkuu Majaliwa pindi alipokuwa anatolea ufafanuzi kuhusiana na suala hilo;