
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mkuu wa Zesco Victor Mapani amesema “kuanzia sasa nyumba zote na makampuni katika nchi nzima yatapata umeme kwa masaa 24 bila usumbufu”.
Bw.Mapani ameeleza kuwa suluhu hiyo imepatikana kutokana na njia tofauti zikiwemo kuboreshwa kwa uzalishaji wa umeme katika vituo mbalimbali nchini humo na kuboreshwa kwa kituo cha umeme cha maporomoko ya Victoria.
Vilevile Bw.Mapani ameongeza kwa kusema kuwa hivi karibuni Zesco itaongeza uzalishaji wa umeme kwenye ziwa Kariba.
Matatizo ya umeme nchini humo yalikuwa yakisababishwa na kushuka kwa kina cha maji kwenye Bwawa la Kariba na matengenezo ya eneo la mgodi wa Maamba.