Sevilla imemfuta kazi kocha Jorge Sampaoli na imemteua Jose Luis Mendilibar kuwa kocha mpya hadi June 2023.
–
Sampaoli aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo mwezi Oktoba mwaka Jana akichukua nafasi ya Julen Lopetegui na alisimamia mechi 31 katika mashindano yote.
ADVERTISEMENT
–
Katika mechi 31 akiwa katika klabu hiyo, amefungwa mechi 12, akitoka sare mechi 6 na kupata ushindi mechi 13 pekee.
–
ADVERTISEMENT
Sevilla italipa ada ya fidia ya zaidi ya Euro milioni 10 kwa kukatisha mkataba wake kabla ya wakati, mkataba wa Sevilla na Jorge Sampaoli ulikuwa unafikia tamati June 2024.