Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35-40 amezua taharuki kwa wakazi wa mtaa wa Mazense A Wilayani kilosa mkoani Morogoro baada ya kujitumbukiza kwenye kisima cha Maji chenye urefu wa zaidi ya mita 20 ambacho maji yake hutumika na wakazi hao kwa matumizi mbalimbali.
–
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mtu huyo alifika katika kisima cha kwanza na kukuta watu wanachota maji kisha kutaka kuzama kisimani lakini wananchi walimkataza lakini badae aliondoka kwenda kisima kingine na kujiyumbukiza humo.
–
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Mazensa A Mashaka Ally amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wamefanikiwa kumtoa mtu huyo akiwa hai na alipohojiwa alisema ameamua kuchukua maamuzi hayo kwa sababu ya maisha magumu
–
Aidha mwenyekiti amebainisha kuwa kwa sasa amempeleka mtu huyo hospitali ili kupata matibabu pamoja na vipimo vingine.