Kaimu mkurugenzi Mamlaka ya MajiSafi na usafi wa mazingira Morogoro ( MORUWASA) Lyang’onjo Kiguhe amesema Kwa kipindi cha mwezi januari pekee mwaka huu Dira za maji 52 zimeibwa katika maeneo Mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro na kuleta hasara zaidi ya milioni tano Kwa mamlaka hiyo.
–
Kutokana na chamgamoto hiyo mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Morogoro ( MORUWASA) wamekutana na wanunuzi wa chumachakavu Manispaa ya Morogoro ili Kuwapa elimu namna ya kutambua Mali za mamlaka hiyo na kushiriki kuwakamata wezi wa miundombinu hiyo.
–
Mwanasheria wa MORUWASA Tumain Kimaro anasema Kwa Mtu yoyote atakayekamatwa Kwa kuharibu au kuiba vifaa vya maji na Uchepushaji atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na anaweza kulipa faini kuanzia laki tano Hadi milioni 50 au kifungo cha miaka mitano.
–
Anasema mamlaka hiyo Kwa sasa imedhamiria katika kulinda rasilimali za maji hivyo mpango ni kuendelea kusimamia Sheria zilizopo ili kuisaidia kuondokana na hasara zisizo za lazma
–
Baadhi ya wauza vyuma chakavu mkoani Morogoro wamesema awali walikua hawafahamu madhara ya kununua vitu hovyo lakin kupitia elimu waliyopatiwa watakua walinzi kwa Kutoa taarifa kwenye uongozi pindi watakapo letewa vifaa hivyo na wezi
–
Kwa upande wa afisa mnadhimu wa jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro Hassan Omary amesema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana wananchi ili kuinua watu wanaofanya uharibifu na wizi miundombinu ya maji.
–
Omary ameongeza kuwa hadi sasa watu saba wamekamatwa ambapo watano kati yao wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kuharibu miundombinu ya maji.