Kiungo wa Yanga na Burkina Faso, Stephane Aziz Ki amejumuishwa katika safu ya viungo saba wanaounda kikosi cha wachezaji 24 wa timu ya Taifa ya nchi hiyo.
–
Burkina Faso inaingia kambini kujiandaa na mchezo wa kundi B kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) dhidi ya Togo ambayo itapigwa Machi 24, 2023.
–
ADVERTISEMENT
Wakati huo huo, kiungo wa Simba na Burundi, Saidi Ntibanzonkiza naye ameitwa kambini kujiandaa na mashindano hayo.
–
Intamba mu Rugamba itashuka dimbani katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya na Indonesia.
–
CREDIT : TBC