Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema Serikali kuzuia mtoto wa umri wa miaka 14 kuolewa ni kuzuia kumuabudu Mungu na kumruhusu shetani aingie kati.
–
Akizungumza na Swahili Times, Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikhe Hassan Chizenga amepinga kubadilishwa kwa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, hasa kipengele kinachoruhusu binti wa miaka 14 kuolewa kwa idhini ya mahakama katika mazingira maalum.
–
“Ndoa ina maana mtoto wa kike na wa kiume waruhusiwe kufanya tendo la ndoa, wawe wapenzi. Ikifanywa akatajwa Mungu na usimamizi wa wazazi kosa, lakini ikifanywa kiholela bila usimamizi wa wazazi ni sawa, mimi naona hiki ni.. [akitaja neno kali].
–
Kama Serikali inagawa kondumu ili kuwakinga na maambukizi, hivyo basi imekubali ndoa ya shetani iwepo lakini ya Mungu isiwepo. Sera ya nchi yetu inakubaliana kwamba haja ya kufanya hivyo [kujamiiana] ipo,” amesema.
–
Aidha, amesema dini haijataka kila mtoto aozeshwe akiwa na umri wa miaka 14, ila pale dharura itakapolazimu basi asizuiwe na kulazimishwa kuzini kwa sababu sheria inamlazimu.
–
Chanzo ; Swahili Times