ADVERTISEMENT

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limeandaa hafla ya tuzo za wanamichezo bora nchini ambayo imepangwa kufanyika Machi 17 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Mwenyekiti wa BMT Leordegar Tenga,alisema kuwa lengo ni kutambua,kuongeza na kuenzi wanamichezo na timu za kitanzania zilizofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa .
Àlisema kuwa hafla hiyo itatumika kutambua mchango wa wadau wanaosaidia katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya michezo nchini.
“Baraza limeona sasa ni wakati muafaka kuanza kutambua na kuwapongeza wanamichezo na timu za kitanzania zinazofanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa pamoja kuitangaza nchibyetu kimataifa,” alisema Tenga.

Àlisema tuzo zitatoa tuzo aina tatu ikiwamo wanamichezo waliofanya vizuri katika michezo mbalimbali,timu zilizofanya vizuri kimataifa ,na mwanamichezo bora wa kiume na kike, mwanamichezo bora mwenye Ulemavu wa kike na kiume , mchezaji bora kutoka katika skuli wa kike na kiume.
Alibainisha kuwa vigezo vya kuingia katika tuzo hizo ni pamoja na ushiriki wa kufanya vizuri kimataifa ,Kanda ,Afrika na Dunia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo Profesa Mkumbukwa Mtambo,aliomba wanahabari kushiriki katika kuhamasisha jambo hilo.
Àlisema kuwa lengo ni kuhamasisha walioofafanya vizuri Ili wafanye vizuri zaidi na wasiofanya wafanye vizuri.
ADVERTISEMENT