ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, June 9, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

I am Krantz by I am Krantz
Mar 24, 2023
in HABARI
0
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
0
SHARES
41
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias akishuhudia mteja Dosian Augustine akifanya muamala  katika mashine ya ATM ya Tawi la Mlimani City mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC inayolenga kuwapa watumiaji wa ATM za NBC nafasi ya kujishindia Zawadi na kuweza kuwa sehemu ya kufurahia Udhamini wa Benki ya NBC kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

 

Meneja wa Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Lilian Mutalemwa akitoa zawadi ya Jezi kwa mmoja wa washindi wa Kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC Dosian Augustine baada ya kushinda alipofanya muamala wake katika mashine ya ATM Mapema leo.
Meneja wa Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Lilian Mutalemwa akitoa zawadi ya mpira  kwa mmoja wa washindi wa Kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC Bi Rehema Mushi baada ya kushinda alipofanya muamala wake katika mashine ya ATM Mapema leo.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya NBC na wateja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC katika hafla iliyofanyika mapema leo katika Tawi la Mlimani city

Dar es Salaam.Machi 24,2023- Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC inayolenga kuwapa watumiaji wa ATM za NBC nafasi ya kujishindia Zawadi na kuweza kuwa sehemu ya kufurahia Udhamini wa Benki ya NBC kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Zawadi za kusisimua, ikiwa ni pamoja na tiketi za kushuhudia mechi za Ligi kuu ya Mabingwa ya NBC, jezi, na zawadi nyingine kemkem.

RelatedPosts

KARIM BENZEMA ATAMBULISHWA RASMI AL-ITTIHAD

KARIM BENZEMA ATAMBULISHWA RASMI AL-ITTIHAD

Jun 9, 2023

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 9, 2023

Jun 9, 2023

TRA YAUJUZA UMMA KUWA USAJILI WA TIN INAYOSISITIZWA NI KAMA NIDA, SIO ILE YA BIASHARA

Jun 8, 2023
Load More
Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC Bw, David Raymond, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC zilzofanyika mapema leo katika tawi la Mlimani city.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC Bw, David Raymond, alisema, Kampeni hii ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC inalenga kuhamasisha wateja wa NBC na wasio wateja wa NBC kutumia mashine za ATM za NBC kufanya miamala yao. Wateja ambao watatumia kadi zao za ATM kufanya miamala mbalimbali katika kipindi cha kampeni watapata nafasi ya kushinda zawadi za kusisimua, ikiwa ni pamoja na tiketi za kushuhudia Ligi ya Mabingwa ya NBC, Jezi, na zawadi nyingine kemkem.

“Tunayo  furaha kuzindua kampeni hii ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC ambayo inawazawadia watumiaji wote wa ATM za NBC ikiwa ni wateja wa NBC na wasio wateja wa NBC.Tunaelewa umuhimu wa urahisi katika huduma za benki, tunazidi kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja kwa kuongeza ATM mpya kwenye maeneo mbali mbali nchini. Watumiaji wa ATM za NBC wanaweza kuweka pesa kwenye akaunti yoyote ya NBC kupitia ATM zilizopo kwenye matawi yetu nchi nzima. Alisema David

Aliongeza “Pia wale wasiokuwa na akaunti yoyote wanaotumiwa fedha kwa kutumia huduma ya NBC Cash Popote, wanaweza kutoa pesa hizo kwenye ATM yoyote ya NBC. Wote walio na kadi za VISA, Union Pay na Mastercard wanaweza kutumia ATM za NBC kutoa pesa. Makundi yote haya yanayo nafasi sawa ya kujishindia Zawadi hizi katika kampeni hii. Tunaamini kuwa watumiaji wa ATM za NBC wataendelea kufurahia huduma zetu, tunawakaribisha wote watumie ATM za NBC.”

ADVERTISEMENT
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias.  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC zilzofanyika mapema leo katika tawi la Mlimani city.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias aliongeza kuwa zawadi hizo zitakuwa ni za papo kwa papo, pale mteja akifanya muamala wake kwa kutumia ATM ya NBC atapata kujua kuwa ameshinda zawadi gani kwa kuangalia nyuma ya risiti ya muamala wake.

“Sisi kama benki ya NBC, daima tunawaweka wateja wetu karibu na kuhakikisha wanafurahia huduma zetu wakati wowote na popote. Kampeni yetu ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC Tunafurahi kuwapa  wateja wetu nafasi ya kushinda tiketi za kuona Ligi ya Mabingwa, jezi, na vitu vingine vya kumbukumbu ya Ligi ya NBC. Tunatumai kuwa kampeni hii itaimarisha zaidi uhusiano wetu na wateja wetu pamoja na watumiaji wote wa ATM zetu.” alisema Urlik

Kampeni hii inawalenga watumiaji wote wa ATM za Benki ya NBC za Dar es Salaam na Kibaha. Kila mtumiaji wa ATM za NBC akishafanya muamala, achukue risiti yake, aigeuze nyuma kuangalia zawadi aliyoshinda. Kisha aende na risiti yake kwenye tawi lolote lililo karibu naye ili kuchukua zawadi yake. Tukio hili lilihudhuriwa na wateja wa NBC na wanahabari ambao walipata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu kampeni hii ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC na kuzungumza na wafanyakazi wa NBC.

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 9, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 9, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 9, 2023
TRA YAUJUZA UMMA KUWA USAJILI WA TIN INAYOSISITIZWA NI KAMA NIDA, SIO ILE YA BIASHARA
HABARI

TRA YAUJUZA UMMA KUWA USAJILI WA TIN INAYOSISITIZWA NI KAMA NIDA, SIO ILE YA BIASHARA

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
DR. MPANGO ATILIA MKAZO JITIHADA ZA KULINDA HIFADHI YA BAHARI NA RASILIMALI ZAKE
HABARI

DR. MPANGO ATILIA MKAZO JITIHADA ZA KULINDA HIFADHI YA BAHARI NA RASILIMALI ZAKE

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
EWURA YATOA BEI HII KIKOMO YA MAFUTA NCHINI
HABARI

EWURA YATOA BEI HII KIKOMO YA MAFUTA NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI HUU LEO
HABARI

RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI HUU MPYA LEO

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
MESSI AFUNGUKA SABABU ZA KUIPOTEZEA BARCA
HABARI

MESSI AFUNGUKA SABABU ZA KUIPOTEZEA BARCA

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In