Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu Burna Boy anatarijiwa kutumbuiza kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya itakayofanyika nchini Uturuki.
–
UEFA Champions League kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wamethibisha kuwa Burna Boy ni miongoni mwa wanamuziki watakaotumbuiza katika Fainali itakayofanyika Jumamosi, June 10, 2023 kwenye uwanja wa Atatürk Olympic mjini, Istanbul nchini Uturuki.
–
“Habari njema! Burna Boy atatumbuiza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Istanbul” sehemu ya jumbe wa UEFA Champions League katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.
–
Mwaka huu umeanza vizuri kwa upande wa Burna Boy kwani Hivi karibuni alitumbuiza kwenye Mechi ya NBA All-Star.