Chelsea FC itakuwa Klabu ya kwanza kutoka Premier League kuandaa Futari kwaajili ya Waislamu watakao kuwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mkukufu wa Ramadhan.
–
Tukio hilo la kihistoria litafanyika Machi 26, kwenye Uwanja wa Stamford Bridge lengo likiwa ni kukuza uvumilivu wa kidini na kuleta umoja.
–
Kufuturisha wakati wa Ramadhan litakuwa ni tukio kubwa zaidi katika jamii ya Uingereza, itaruhusu Waislamu kukusanyika na kufungua mfungo wao pamoja.
–
Hafla hiyo itahusisha Misikiti ya karibu na Klabu hiyo, Wanachama na Wafanyakazi wa Chelsea wa imani ya Kiislamu, itawaleta watu pamoja na kukuza uelewa wa Ramadhan.