Nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuwa mmoja wa wageni waalikwa katika mashindano ya Formula 1 Grand Prix mjini Jeddah wikendi hii.
ADVERTISEMENT
–
Katika mkataba wake na klabu ya Al-Nassr una kifungu ambacho kinamtaka Ronaldo kuwepo, wakati wa mbio hizo za Formula 1 Grand Prix ya Saudi Arabia.
–
ADVERTISEMENT
Al Nassr itakuwa na mchezo siku ya Jumamosi na klabu ya Abha katika muendelezo wa Ligi ya Saudi Pro League huku mbio hizo za Formula 1 Grand Prix zikitarajiwa kufanyika siku ya Jumapili.