ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, June 2, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Dk. Mpango aipongeza NMB kampeni ya Upandaji Miti, Shule zatengewa Mil. 472/-

I am Krantz by I am Krantz
Mar 29, 2023
in HABARI
0
Dk. Mpango aipongeza NMB kampeni ya Upandaji Miti, Shule zatengewa Mil. 472/-
0
SHARES
56
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

Meeting Ladies In Your 30s

Jun 1, 2023

SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF

Jun 1, 2023

RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR

Jun 1, 2023
Load More

 

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Isdor Mpango, ameipongeza Benki ya NMB na kuitaja kuwa kinara katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kupambana na Athari za Mabadiliko ya tabianchi.

Dk. Mpango Ametoa pongezi hizo baada ya NMB kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji Miti Milioni 1 kwa kushirikiana na Wakala huduma za Misitu Tanzania (TFS), huku ikitenga kiasi cha Sh. Milioni 472 kuzizawadia shule zitakazofanya vema katika shindano la utunzaji na uhifadhi wa miti.

Uzinduzi huo sambamba na upandaji wa miti 3,000 ya matunda, kivuli, mbao na dawa, umefanyika katika Mji wa Serikali,  Mtumba, jijini Dodoma, hafla iliyohudhuriwa na mawaziri, viongozi mbalimbali wa Serikali, Wadau wa Mazingira, wanafunzi wa shule na Vyuo Vikuu, watumishi wa benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,  Ruth Zaipuna na Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Edwin Mhede.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Mpango amesema kampeni hiyo chanya inaitia moyo ofisi yake, na kubainisha kuwa kutokana na ukweli kwamba bila miti hakuna mvua, chakula, maji, hewa safi na ndio chanzo cha mafuriko na athari nyingine za Mabadiliko ya Tabianchi, Serikali inahitaji uungwaji mkono kama unaofanywa na NMB.

“kinachofanywa leo na NMB ni cha kuigwa na kupongezwa, kampeni hii inaenda kusapoti pakubwa jitihada za Rais Samia, ambaye amejipambanua katika hili, amekuwa kiongozi mwenye mkazo wa suala la mazingira tangu akiwa waziri, kisha Makamu wa Rais na sasa akiwa Rais wa Tanzania, akitambua kuwa mazingira yanagusa sekta zote kimaendeleo.

“Na kwa mantiki hiyo, nasisitiza kuomba wadau wa mazingira, mashirika, kampuni, taasisi na jamii kwa ujumla, kujitoa katika kumsapoti Rais Samia, kwani Serikali Pekee haiwezi kufanikisha mapambano haya. Ndio maana naipongeza NMB kwa uharaka wao kuitikia wito huo, zaidi kwa kuongeza fungu la Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), sambamba na kubuni shindano la upandaji miti, utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwenye shule zetu.

“Kuna maana kubwa kwa NMB kuongeza Shilingi Bilioni 2 kwenye CSR, ambazo ni maalum kwa ajili ya mazingira, lakini kama haitoshi Ikatenga Sh. Milioni  472 kuzizawadia shule zitakazofanya vema katika shindano la upandaji na utunzaji miti linalozinduliwa sanjari na kampeni hii. Zawadi za shule washindi ni nono na kutokana na uwingi wake na idadi ya wanafunzi,  maana yake elimu inaenda kuifikia jamii kirahisi,” alifafanua Dk. Mpango.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisisitiza kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi hazijawahi kumuacha yeyote salama na kwa kutambua hilo, benki yake ikaongeza fungu lake la CSR kutoka Sh. Bilioni 4.2 (ambazo ni asilimia 1 ya faida yao kwa mwaka Sh. Bil. 429), hadi kufikia Sh. Bilioni 6.2, ongezeko linalothibitisha namna wanavyojali na kuthamini mazingira.

ADVERTISEMENT

Aidha, akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo alisema kuwa wizara yake iko tayari kushirikiana vyema na Benki ya NMB na kuhakikisha kuwa adhma ya kupanda miti milioni moja kwa mwaka 2023 inatimia kikamilifu.

“Wizara yetu haitahakikisha miti hii milioni imepandwa lakini tutahakikisha miti hii yote inkuwa na kustahimili ili iweze kuleta tija katika mazingira yetu na kuwa na manufaa kwetu,” alisema Mhe. Dkt. Jafo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angella Kairuki alimuhakikishia Makamu wa Rais kuwa wizara ya TAMISEMI watahakikisha uratibu wa mashule katika shindano lililoasisiwa na Benki ya NMB unaenda kiufasaha na shule nyingi katika hlamashauri zote nchini zitashiriki.

ADVERTISEMENT

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Edwin Mhede alisema kuwa Benki ya NMB imeamua kuja na kampeni hii kwani ni Ajenda ya kidunia na taasis kama NMB hawana Budi kuja na kampeni kama hii kwani ni jambo lenye manufaa kwa taifa.

Katika hafla hiyo, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo alisema kuwa wata hakikisha wana shirikiana vyema na Benki ya NMB kwa kuwapatia mishe bora ya miti pamoja na utaalamu walionao katika masuala ya miti ili kuhakikisha kampeni ya miti milioni inatimia.

Mwisho

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

HABARI

Meeting Ladies In Your 30s

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF
HABARI

SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR
HABARI

RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
WANAWAKE WAONYWA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAUME
HABARI

WANAWAKE WAONYWA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAUME

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
JINSI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO
HABARI

JINSI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
Customer Service Officer Job Vacancies at TADB
HABARI

Customer Service Officer Job Vacancies at TADB

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In