Mwanasheria wa Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema ni mapema mno kuzungumza lolote kwa sasa, kufuatia maamuzi yaliyotangazwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.
–
Feisal aliomba kurejewa kwa maamuzi ya shauri lake dhidi ya Yanga, lakini bado Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaendelea kusimamia msimamo wake wa kumtambua kama Mchezaji halali wa Klabu hiyo ya Jangwani.
–
Fatma Karume ambaye alikuwa sehemu ya Wanasheria wa Kiungo huyo katika marejeo ya Shauri la Feisal dhidi ya Yanga, amesema wanachosubiri kwa sasa ni nakala ya hukumu ili taratibu nyingine zifuate ikiwa pamoja na kumshauri mteja wake.
–
ADVERTISEMENT
Amesema jambo kubwa na la msingi katika kesi hiyo, ni mteja wake kulazimishwa kuendelea kuitumikia Yanga, ili hali yeye mwenyewe hataki kufanya hivyo, na TFF kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wanapaswa kuzingatia suala hilo.
–
“Tunasubiri nakala ya hukumu kutoka TFF na kisha nitamshauri Fei Toto kama maamuzi yake yatabaki hivyo tutaenda CAS. Tatizo la TFF ni kumlazimisha Fei Toto kucheza Yanga kinyume na sheria za FIFA.. huwezi kumlazimisha mchezaji kucheza Yanga sio mtumwa yule.”
–