Watu 10 katika Kijiji cha Nyamalimbe Kata ya Nyamalimbe Wilayani Geita Mkoani Geita, wamejeruhiwa na Mnyama aina ya Fisi na baadaye fisi huyo kuua Ng’ombe mmoja.
–
Akisimulia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi ACP. Bethaneema Mlayi, amesema baada ya kupata taarifa za fisi huyo walifika eneo la tukio na kukuta wanakijiji wamekusanyika kwa ajili ya kumuua fisi huyo ndipo walichukua uamuzi wa kuwatafuta Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori na Misitu Geita (TFS) kufika eneo hilo na kumuua Fisi huyo.
–
Kaimu Kamanda Bethaneema amesema Fisi huyo amejeruhi watu watano wa familia moja na kwa Ujumla wao wanaendelea vizuri kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kama hali zao zitaimarika kufikia jioni wataruhusiwa kwenda Nyumbani.