Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland baada ya jana kufunga mabao 5 kwenye ushindi wa mabao 7-0 walioupata Man City dhidi ya RB Leipzing kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya UEFA, amefanikiwa kufikisha rekodi zifuatazo;
–
Haaland amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao 5, kwenye mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa Ulaya huku akiungana na Lionel Messi aliyefanya hivyo mwaka 2012 na Luiz Adriano mwaka 2014.
–
ADVERTISEMENT
Pia amefikisha jumla ya Hat-tricks 5 msimu huu kwenye michuano yote, ikiwa ni hat-trick ya 3 zaidi ya mchezaji yoyote kwenye ligi kubwa 5 barani Ulaya msimu huu 2022-23.