Mwanamuziki Phina amesema licha ya kufananishwa kiuimbaji na Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameupa muziki kisogo bado hajamuogopa.
–
The Melanin Queen katika mahojiano na Kituo cha EATV aliulizwa kuhusu nafasi yake kama leo Vee Money anaamua kurudi tena kwenye Muziki, Mwanadada Phina alisema
–
“Nafasi yangu haiwezi kuyumbishwa na mtu yeyote, yeye [Vanessa] ana nafasi yake na mimi nina nafasi yangu kwenye muziki. Kwa hiyo I respect her na vitu alivyofanya, akiamua kurudi nitapenda kufanya naye kazi. lakini siwezi kutishika kwamba nafasi yangu itakuwa hatarini, hapana.”
–
Phina kwa sasa ameachia wimbo unaoitvwa Zinduna kati nyimbo tatu anazotarajia kuziachia ambazo amezipa jina la hat-trickTatu 3.3.3.