Baadhi ya wakazi wa jiji la Istanbul nchini Uturuki wamejawa na hofu juu ya usalama wao baada ya majengo wanayoishi kufeli vipimo vya kiusalama.
–
Majengo hayo yamefanyiwa vipimo ili kupima uwezo wa kustahimili tetemeko la ardhi na baadhi yamekutwa na udhaifu mkubwa.
–
Mkazi mmoja amesema kuwa yeye na familia yake wanalazimika kuhama haraka ili kujihadhari na hatari inayoweza kutokea wakati wowote mana hadi hivi sasa jengo lao tayari linao ufa mkubwa.
–
Asilimia 70 ya majengo katika jiji la Istanbul yalijengwa kabla ya kubadilika kwa sheria za viwango vya ujenzi mwaka 1999 na hivyo kwa sasa yanahesabika kuwa si salama.
–
Matokeo ya utafiti uliofanywa miezi mitatu iliyopita yalieleza kuwa upo uwezekano wa kutokea tetemeko kubwa la ardhi katika mji wa Istanbul kabla ya mwaka 2030, na ikiwa litatokea basi tetemeko hilo linaweza kusababisha takribani watu 90,000 kupoteza maisha.
–
Hivi sasa mji huo uko katika harakati za maandalizi ya kiusalama.