
Gianni Infantino amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa muda wa miaka minne.
–
Infantino mwenye umri wa miaka 52, amepita bila ya kupingwa kwenye kongamano lililofanyika Kigali nchini Rwanda leo siku ya Alhamisi.
–
Mwanasheria huyo ameiongoza FIFA tangu kuondoka kwa utawala wa Joseph Blatter, mnamo mwaka 2016 na bado anayo nafasi ya kuwania tena mwaka 2027.
–
“Kuwa Rais wa FIFA ni heshima kubwa, ninashukuru na kuguswa na sapoti yenu. Nitaendelea kuhudumu FIFA, nitautumikia mpira dunia nzima, nitahudumia mashirikisho yote 211 ya FIFA”, amesema, Infantino.
–
Lakini nchi kadhaa za Ulaya, zikiwemo Ujerumani, Norway na Sweden, hazijafurahishwa na urais wake na zimesema hazitamuunga mkono kikamilifu.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT