Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amewasili nchini kwa ziara ya siku tatu.
–
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Kamala pamoja na ujumbe wake amepokelewa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
–
Akiwa hapa nchini pamoja na mambo mengine, Kamala anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan hapo kesho Machi 30, 2023 Ikulu, Dar es Salaam.
–
Kamala Harris amewasili nchini akitokea nchini Ghana na baada ya kuhitimisha ziara yake Tanzania ataelekea Zambia. Hii ni ziara yake ya kwanza Barani Afrika tangu aliposhika wadhifa huo mwezi Januari mwaka 2021.