Katika kikao cha Baraza la FIFA kilichofanyika jana Machi 14, 2023 huko Kigali, Rwanda, Shirikisho hilo la Mpira Duniani (FIFA) limepitisha mabadiliko mapya ya mfumo wa mechi za Kombe la DUNIA la 2026 litakalo pigwa huko nchini Marekani, Mexico na Canada.
–
FIFA imeamua kuwa kutakuwa na makundi 12 yenye jumla ya timu 48 na kila kundi litakuwa na timu 4 hivyo jumla ya mechi 104 zitapigwa katika nchi hizo za America ya Kaskazini.
–
Awali Kombe la Dunia lilikuwa likihusisha jumla ya makundi 8 yenye jumla ya Timu 32 ambapo kila kundi lilikuwa na jumla ya Timu 4.
–
Aidha FIFA imeainisha kuwa michuano hiyo ya Kombe la DUNIA 2026 itaanza kutimua vumbi siku ya Jumapili, Julai 19, 2026.